Halmashauri zote za wilaya mkoana Tabora,zimeagizwa kuwatumia wanachuo wa chuo cha ardhi katika kupima viwanja kutokana na kuewepo na upungufu wa watumishi wa idara ya Ardi katika Halmashauri hizo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Daktari Agelina Mabula wakati akizungumza na watumishi wa chuo cha Ardhi na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Amesema kuwa kuna tatizo la watumishi katika sekta ya ardhi lakini halmashauri zimekuwa zikishindwa kuw tumia wataalamu wa chuo cha Ardhi Tabora jambo ambalo lingepunguza tatizo lililopo la upimaji ardhi.

Kwa upande wake,Mkuu wa chuo cha Ardhi Tabora, Biseko Musiba amesema wanachuo wengi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa ufanisI wanapokwenda kwenye mazoezi kutokana na vifaa kuwa na bei kubwa na kusababisha washindwe kumudu gharama hizo.

Kocha wa Azam aipania Mwadui
Kichuya aeleza mikakati yake

Comments

comments