Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG, Charles Kichere amesema baada ya ukaguzi, Halmashauri 14 zimepata hati zenye mashaka na huku Ushetu ikipata hati chafu.

CAG Kicheere ameyasema hayo wakati akisilishaji wa ripoti yake hii leo Machi 29, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na kuzitaja Halmashauri zilizopata hati zenye mashaka kuwa ni Arusha, Babati, Bahi, na Geita.

Zingine ni, Kilindi, Mbinga, Musoma, Nkasi, Nyasa, Simanjiro, Songwe, Sumbawanga na Ushetu iliyopata hati mbaya huku katika vyama vya siasa, Chama cha Sau kilipata hati chafu, Demokrasia Makini, UDP, Chama cha wakulima vikipata hati zisizoridhisha.

Kwa upande wa mashirika ya umma ni Magazeti ya Serikali, Kampuni ya mbolea, mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Nzega, Korogwe na Kyela-Kasumuru, Taasisi ya Mifupa Muhimbili, Shirika la Masoko ya Kariakoo.

TANAPA kujiuliza matumizi fedha za UVIKO-19
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 29, 2023