Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Aprili 29, 2021 wamefanya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Jijini Dodoma, kwa ajili ya kuandaa Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika kesho Aprili 30, 2021.

Wajumbe 1876 wa mkutano mkuu maalumu wa CCM wanatarajiwa kupigia kura jina moja litakalowasilishwa katika mkutano huo kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho tawala nchini.

Mkutano huo unafanyika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kufariki dunia Machi 17,2021 na atakayechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho baada ya kifo cha Magufuli, mchakato wa kumpata Mwenyekiti mwingine uliendelea kufanyika na kesho ndio unafanyika uchaguzi huo.

Uwanja utakaochezwa fainali ligi ya mabingwa kujulikana kesho
Serikali kutekeleza uwekezaji mto msimbazi