Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa onyo kwa halmashauri kutoa mikopo kwenye vikundi hewa na kwa watu ambao sio walengwa wa mikopo hiyo.

Waziri Bashungwa ameagiza wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji ambayo inakusanya mapato zaidi ya Sh bilioni 5, kutenga na kutoa fedha asilimia 10 kwa ajili ya kuimarisha barabara za mitaa.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

” Baada ya mafunzo haya, masuala ya vikundi hewa lazima yajadiliwe na tutoke na mkakati wa kuyadhibiti, ili iwe ni historia tusisikie mambo ya vikundi hewa” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesisitiza kuwa waliopewa mafunzo hayo wahakikishe wanafuatilia mikopo iliyotolewa kwa vikundi ili kuwe na tija na mkopo ubadilishe maisha ya wanufaika.

“Kwanza nishukuru kwa kuja na mfumo huu na ni njia sahihi ya kutekeleza maelekezo ya CAG kwenye maeneo ambayo tumeelekezwa upande wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI hususani ni kwenye fedha za asilimia 10 na usimamizi wake limekuwa ni hoja inayojirudia kwa CAG lakini na Bunge kupitia Kamati za LAAC na USEMI limekuwa likitoa maoni na mapendekezo kila mwaka ni hayo hayo.”

Sasa Changamoto hizi zimefika mwisho niwataka Mamlaka zote za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatumia vyema mfumo huu katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Chaneli rasmi ya mtandao wa YouTube ya Dar24 Media imerudi hewani
Mataifa kujadili uhalali biashara ya Pembe za Ndovu