Aliyekuwa mwanachama wa CUF, Hamad Rashid ambaye hivi karibuni alijiunga rasmi na chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) amerusha jiwe kwa chama chake hicho cha zamani akidai kuwa kinafanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa rasmi kadi ya chama cha ADC na mwenyekiti wa chama, Said Miraj, Hamad Rashid alieleza kuwa Chama Cha Wananchi CUF kilipoteza muelekeo wake baada ya kufikia muafaka na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alieleza kuwa baada ya kuingia katika serikali ya Zanzibar, CUF iliacha kutekeleza manifesto yake na kuanza kutekeleza Ilani ya CCM.

“Baada ya muafaka ambao ulichezewa hapo katikati, ikaundwa serikali ya umoja wa kitafa. Serikali ya umoja wa kitaifa ilitegemewa kwanza ingekuwa na manifesto ya pamoja. Kwa hiyo serikali ya umoja wa kitaifa ikatekeleza ilani ya CCM. Ukiwauliza CUF manifesto yenu ya mwaka 2010/2015 iko wapi, hawanayo kwa sababu walikuwa wanatekeleza ilani ya CCM,” Alisema.

Aidha, Hamad Rashid ambaye ametangaza kugombea Urais kupitia ADC, alisema endapo atapewa nafasi ya kuiongoza serikali, atahakikisha serikali yake inainua kipato cha wananchi masikini na kuwa na uchumi wa kati. Katika kufanikisha hilo, mwanasiasa huyo alisema kuwa serikali yake itashirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kufufua uchumi wa nchi.

Lembeli Ataja Kiasi Alichotaka Kuhongwa Asilipue ‘Operesheni Tokomeza’
Aliyebaguliwa Ufaransa Achachamaa