Benchi la ufundi la mabingwa wa kombe la shirikisho (ASFC) Azam FC limempatia programu maalumu ya mazoezi mchezaji wake aliyesajiliwa katika dirisha dogo la mwezi Januari, Khleffin Hamdoun ili kuzoea utamaduni wa Azam FC na kuongeza ujuzi wake baada ya kuonekana kukosa nafasi ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe.

Hamdoun alikamilisha usajili wake kutokea Klabu ya Mlandege Januari 8, mwaka huu na kusaini mkataba wa miaka minne kuitumikia Azam lakini ameonekana kupata wakati mgumu kuzoea mazingira.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam Zakaria Thabith ‘zaka za kazi’ amesema kuwa benchi la ufundi limempa programu maalumu mchezaji huyo ambayo itamsaidia kukuza kipaji chake.

“Hamdoun ni kijana mdogo ambaye ana mengi ya kujifunza bado, hivyo kocha amempatia programu maalumu ya kumwezesha kukuza kipaji chake na kumjengea ule utamaduni wa Azam.

“Hii ni kumwandaa ili atakapoingia rasmi kwenye kikosi aweze kufanya yale makubwa ambayo wadau na wapenzi wa Azam wanayasubiri kutoka kwake,” alisema Thabith

Error: Contact form not found.

Wagonjwa wawili wa Covid 19 wathibitika Burundi
EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta