Mshambuliaji kutoka nchini Uganda na klabu ya Kagera Sugar Hamis Kiiza ‘Diego’ amesema anatarajia mchezo mgumu dhidi ya Simba SC leo Jumatano (Mei 11), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC iliyopoteza mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba mkoani Kagera, itakua mwenyeji wa mchezo huo wa Mzunguuko wa Pili ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wengi wa Soka nchini.

Kiiza amesema Simba SC imebadilika kwa kiasi kikubwa na itaingia Uwanjani ikiwa na lengo la kutorudia makosa walioyafanya kwenye mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza, hivyo kwa hali hiyo anaamini kazi itakua kubwa.

Mshambuliaji huyo ambaye aliifungia Kagera Sugar bao pekee na la Ushindi kwenye mchezo wa Mzunguuko wa kwanza dhidi ya Simba SC, amesema wamejiandaa kukabiliana na hali ya ushindini baadae hii leo, na wana imani kubwa wataweza kuzima mipango ya wenyeji wao.

“Naamini mchezo utakua mgumu sana, Simba SC haitakua tayari kurudia makosa walioyafanya Kagera, wataingia Uwanjani kwa lengo la kupambana ili wapate ushindi, sisi tumejiandaa kukabiliana nao kwa kila hali.”

“Hata sisi tumejiandaa kushinda huo mchezo kwa sababu tunajua tukishinda leo tutakua kwenye nafasi gani katika msimamo, kwa hiyo hivi vitu vinakuonyesha mchezo utakua ni wa aina gani, mchezo utakua mgumu sana.”

“Halafu kitu kingine sisi tumetoka kupoteza mchezo dhidi ya Geita Gold, hili nalo linaongeza ushindani katika mchezo huu, natarajia mambo yatakua magumu sana tena sana, kikubwa mashabiki waje waangalie maana itakua shughuli kubwa sana kati yetu na Simba SC.” amesema Hamis Kiiza

Simba SC inashuka Dimbani SC ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Barakwa kufikisha alama 46, huku Kagera Sugar iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold kwa kufungwa 1-0 ipo nafasi ya 7 kwa kufikisha alama 29.

Patrick Odhiambo aiibia siri Dodoma Jiji FC
Wanaume 2 na mwanamke 1 wakutwa 'Logde' wamefariki huku wameshikana