Mapema leo hii mwanamitindo maarufu nchini aliyezaa na Diamond Platinumz, Hamisa Mobetto amefunguka na kumtaka msanii huyo kuongea na familia yake juu ya mambo yanayoendelea mtandaoni akionesha hapendezwi na maneno yanayoongelewa na ndugu wa karibu Diamond  juu yake.

Mvurugano huu ni kufuatia ujio wa nyimbo ya Iyena ambao umeibua mambo mengi yaliyofichika ndani ya familia ya msanii huyo mkubwa nchini na nje ya nchi Diamond Platinumz.

Ambapo kupitia mtandao wa Instagram Hamisa amefunguka mazito na kufikia kuandika hayo.

”Na tena saa ingine na kaa kimya kuwasitiri kwa mengi na pia @deedylan akikua asione hii migogoro lakini ndugu zako hawabebeki its too much talk to your familia maana wewe ni mwanaume na unauwezo wa kuyamaliza, Na pia waambie unahitaji mke na sio house girl wa nyumba, mwanamke kazi yake kukupikia ule  au nilikua sikupikii tena sio wewe tu ndugu zako mkala na kusaza, leo imekuwa Hamisa hajui kupika, kusafisha nyumba kwahiyo chumba chako tukimaliza lalana huwa anasafisha nani? au walitaka niende kuwafulia vyupi vyao nikimaliza niwapigie deki mpaka chumbani kwao? wakishindwa kuniheshimu basi waambie waheshimu damu yako” amemalizia hivyo.

Hamisa amefunguka hayo kupitia maneno mbalimbali yaliyozuka mtandaoni na ndugu wa karibu wa Diamond wakidai kuwa wamemkumbuka sana Zari Hassan kwani alikuwa mwanamke msafi na pia wanamkumbuka Wema Sepetu kwa kuwa alikuwa mwanamke anayejua kupika chakula, huku wakimsema Hamissa kuwa hajui kufanya kazi za nyumbani.

Hata hivyo siku za nyuma mama mzazi wa Diamond Platinumz, Bi Sandra amewahi kuhojiwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini alisikika akisema siku ambayo mwanaye atafunga ndoa na Hamissa hatohudhuria ndoa hiyo kwa madai kuwa mwanamitindo huyo si mwanamke wa kuoa na kuweka ndani kama mke.

 

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Uswisi
Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari