Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Hamisa Mobetto na mwanzilishi wa Taasisi ya kutoa misaada inayojulikana kama Mobetto Foundation jana Juni 14, 2018 amefuturisha watoto yatima wa kituo cha Chakuwama kilichopo Sinza.

Ambapo mbali na kuwafuturisha watoto hao Mobetto Faoundation ilifanikiwa kupeleka misaada mbalimbali ikiwemu, vyakula, kama vile mchele, unga, pamoja na vinywaji na mahitaji mengine ya kila iku kama sabuni.

Leo kupitia ukurasa wa Instagram wa Mwanamitindo huyo Hamisa Mobetto ametoa shukrani za dhati kwa timu yake nzima iliyosaidia kufanikisha jambo hilo la kheri.

Bila kumsahau Baba mtoto wake, Diamond Platinumz kwa sapoti kubwa aliyompa kwa kuidhamini shughuli hiyo na kutoa mchango wake mkubwa kuifanikisha.

Aidha muwakilishi wa watoto wa kituo hicho alitoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Mobetto Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwakumbuka watoto hao wasio na wazazi na kusema kuwa wamefarijika sana kwa ujio wao na Mungu awalinde na awazidishie kwa vile ambavyo wamejitoa kwa ajili yao.

Mwisho kabisa watoto wa kituo cha Chakuwama wameiombea dua maalumu familia ya Mobetto ikiwa ni sehemu ya Ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Video: Ninayo mengi zaidi ya kumueleza JPM- Mzee Mashaushi
Video: Simbachawene afunguka makubwa kuhusu JPM

Comments

comments