Mara baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kuachia ngoma yake aliyoiita Madam Hero inayohamasisha wanawake kupambana na kuachana na njia za panya, Mobetto amaeahidi pesa yeyote itakayopatikana katika ngoma hiyo atawapelekea wamama wanaolea watoto katika maisha magumu au wale waliojifungua katika hali ngumu.

Amesema hivi karibuni ataachia ngoma hiyo kwanye App mbalimba za muziki ili aweze kuingiza pesa kwa ajili ya kutimiza lengo lake la kuwasaidia kina mama hao.

Aidha kupitia wimbo huo Mobeto ameandika amepitia mambo mengi sana ambayo haoni sababu ya kumlaumi mtu mwingine wala kulalamika kwani anaamini hakuna anayejua ukweli juu ya maisha yake.

Ameongezea kuwa hakupanga maisha yake yawe kama ambavyo yapo sasa ila anaamini Mwenyezi Mungu yake kumpitisha katika mapito hayo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram amaeandika.

”I have been through alot kusema ukweli, lakini pia sioni wa kumlaumu wala haja ya kulalamika kwa sababu anaejua ukweli zaidi ya mie muhusika mweneywe, But naamini kutoa tabasamu kwa jamii inayonizinunguka, wamama wanaonizunguka na kina dada wanaonizunguka, sikupanga njia yangu iwe hii but naona Mwenyezi Mungu anasababu zake ”. Hamisa.

Aidha amewaomba mashabiki wake kuupokea vyema wimbo wake ambao ameuachia hivi karibuni ili uweze kufanya vizuri

Rais Mnangagwa aanza safari kurejea nchini kwake
Video: Hamisa afuata nyayo za Diamond, aachia ngoma yake ya kwanza 'Madam Hero'

Comments

comments