Mwanamitindo Hamisa Mobeto amepigia mstari gumzo lililoibuka wiki kadhaa zilizopita kuhusu matumizi ya nguvu za giza kwenye uhusiano wa mapenzi.

Mrembo huyo ambaye aliwekwa kitimoto kutokana na kuvuja kwa sauti zake ambazo baba wa mtoto wake, Diamond na familia yake walidai alikuwa anaongea na mganga kuroga ili apendwe; amesema kuwa ingawa hakuwa anazungumza na mganga lakini baadhi ya wanaume walimtafuta wakimtaka awaroge.

Akifunguka kupitia The Playlist ya Times Fm wiki iliyopita, alisema kuwa wanaume kadhaa ambao aliwahi kuwa na uhusiano nao, walimpigia baada ya kusikia mkasa huo wakimtaka awaroge wao ili wampende na kufunga naye pingu za maisha.

“Wanaume wengi wanapenda kurongwa[ili wapende],” Hamisa alimwambia Lil Ommy wa Times Fm. “Kuna X wangu alinipigia akaniambia ‘Hamisa si uniroge mimi nikupende, nikupe [pesa] na tuoane,” aliongeza.

Aidha, Hamisa alikiri kuwa sauti zilizosambaa katika mkasa ule ni za kwake na kwamba alikuwa anazungumza na Ostadh kwa ajili ya kufanyiwa dua ili arejee katika amani na mama yake Diamond, na ikiwezekana waoane.

Alisema kwakuwa yeye ni Muislam, kwa imani yake ni kawaida kufanya dua ili maisha yawe ya amani na kwamba alichokuwa anakiomba ni jambo la kheri la kumfanya awe na amani na bibi wa mtoto wake pamoja na familia yake.

 Lil Wayne aachia albamu yake 'the carter v'
CUF waipigia goti Chadema

Comments

comments