Uongozi wa klabu ya Simba umesema kiungo wao wa kimataifa wa Zimbabwe Justice Majabvi kama anataka kuondoka kwenye klabu hiyo ni ruksa kufanya hivyo kutokana na mgogoro uliopo kati ya uongozi na nyota huyo wa nafasi ya ukabaji kwenye kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe amesema hata kama kuna vitu hawajatimiza kwa mchezaji huyo, hatakiwi kwenda kuzungumza nje ya klabu kwasababu mkataba wake unamzuia yeye kwenda kuzungumza nje na kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai hakai yake huko.

“Aende zake tu kwani tunatabu gani sisi. Kama kuna vitu tumetimiza au hatujatimiza hatakiwi kwenda kuanza kupayuka maneno hadharani na mkataba unamnyima yeye nafasi ya kwenda kuzungumza na vyombo vya hari, yeye kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai huko”, amesema Hans Poppe boss wa usajili wa klabu ya Simba.

Majabvi hajasafiri na kikosi cha Simba kilichoelekea Mwanza kucheza dhidi ya Toto Africans kwa madai kwamba haridhishwi na namna kikosi hicho kinavyoendeshwa na inatajwa kuwa kuna matatizo ya ndani kwa ndani kati ya uongozi wa Simba na mchezaji huyo.

Ben Pol ampa 'makavu' Ali Kiba
Niyonzima Afungiwa Kucheza Soka La Bongo