Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na mkandarasi wa uwanja wa klabu hiyo, Frank Peter Lauwo wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha, inayomkabili Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo imetoa amri ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao ili kufika mahakamani hapo kujibu mashtaka.

Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Swai alidai kuwa, amewatafuta washitakiwa hao tangu mwezi Machi mwaka huu  bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Akisoma mashitaka hayo, Swai amedai kwamba, katika shitaka la kwanza, Aveva na Nyange, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka vibaya na kati ya Machi 10 na 16 jijini Dar es Salaam, walitumia madaraka yao vibaya.

Machi 15 mwaka 2016 wanadaiwa kuandaa fomu ya maombi ya kuhamisha dola za Kimarekani 300,000, karibu Sh. Milioni 700 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyopo CRDB tawi la Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Barclays kwa madhumuni ya kujipatia faida.

Aidha, wote kwa pamoja waliwasilisha nyaraka ya kughushi, inadaiwa kuwa Aveva Machi 15, 2016 katika banki ya CRDB aliwasilisha nyaraka ya uongo ikionyesha Simba wanalipa mkopo wa dola za Kimarekani 300,000, takriban Sh. Milioni 700.

Katika shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, imedaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni, Dar es Salaam alijipatia dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Katika shitaka la sita, imedaiwa Nyange alimsaidia Aveva kujipapatia dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi.

Katika shitaka la saba la kughushi, linaloqakabili mstakiwa wa Aveva, Nyange na Poppe imedaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pomoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28/ 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola za Marekani 40,577, ambazo ni zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Katika shitaka la nane imedaiwa Aveva aliwasilisha hati ya madai (commercial invoice),  ya uongo kwa Levison Kasulwa ya Mei 28/ 2016 kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za Marekani 40,577

Katika shitaka la tisa, Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za Kimarekani 40,577.

 

Mussa Mgosi: Simba ilistahili kushinda 6-0
Trump atishia kuifunga tena Serikali kuu ya Marekani