Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesisitiza, lazima Young Africans wapate barua kutoka Simba ili beki Hassan Kessy awe huru kuichezea klabu hiyo ya Jangwani.

Hans Poppe amesema kipindi cha kuidhinisha usajili kwa Tanzania Bara hakijawadia, hivyo lazima kuwe na barua ya ruhusa kutoka Simba ili Young Africans ianze kumtumia katika Kombe la Shirikisho.

“Yanga wao ni watu wabishi, wanajiona wako juu ya sheria. Hili lingeweza kwisha mapema kabisa, lakini hawakutaka kusikiliza.

“Tuliwaeleza mapema hilo la Kessy, lakini waliona wanaweza kupita njia ya mkato. Wanasema wao ni timu ya wananchi, ok,” alisema Hans Poppe.

Young Africans iliamua kutowatumia wachezaji wake wake akiwemo Kessy, Andrer Vicent, Juma Mahadhi na Beno Kakolanya kwa kuwa haikuwa na uhakika kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo kumekuwa na kauli za kuchanganya, awali CAF ilisema ni lazima kupata barua kutoka timu aliyotoka. Kauli ya pili kutoka kwa msemaji wa shirikisho hilo ikaeleza wanaweza kuwatumia lakini lazima iwe makini hasa kama kila kitu kipo kwenye msitari.

Lakini katika mechi dhidi ya Mo Bejaia, Young Africans iliamua kuchukua tahadhari kwa kutomtumia Kessy na wenzake ili kuhakikisha inaondoa hofu hiyo.

Saba wafariki Dodoma kwa ugonjwa usiiojulikana
Mcameroon Kumsabidili Romelo Lulaku