Kocha mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans, Hans van der Pluijm, amesema hahofii chochote kuhusu mabadiliko ya benchi la ufundi yanayozungumzwa na anaelekeza akili yake kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar .

Kesho jumatano Young Africans watakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania Bara, mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam  ambapo Pluijm  alisisitiza kuhusu kufahamu umuhimu wa kushinda mchezo huo.

“Nimesoma kwenye magazeti jana na leo, lakini sijali hizo taarifa. Mwajiri wangu hajaniambia

Na kuhusu mchezo wa kesho, Pluijm alisema awali alikuwa anajua ni Alhamisi, lakini jana ndiyo kaambiwa kwamba ni Jumatano.

Hata hivyo, Mholanzi huyo amesema hana namna nyingine zaidi ya kujiandaa kwa mchezo huo ambao ni muhimu kushinda ili kurejesha imani ya mashabiki katika mbio za kutetea ubingwa.

Habari za ndani kutoka Young Africans, zinaeleza kwamba benchi lote la ufundi litavunjwa na zitakuja sura mpya kabisa baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.

Pluijm na wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wataondoka na Mzambia, George Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

Pluijm amejikuta katika wakati mgumu baada ya Young Africans kuambulia pointi 11 kati ya 18 za michezo sita ya ligi kuu ya Tanzania Bara.

Young Africans imetoa sare mbili, imefungwa mchezo mmoja na kushinda mitatu tangu kuanza kwa ligi kuu – hiyo ikiwa ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Azam kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2.

Wakati Oktoba Mosi, mwaka huu wakilazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu wao, Simba waliokuwa pungufu kwa sehemu kubwa kufuatia nahodha wao, Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29.

Juuko Aungana Na Wenzake Jijini Mbeya
Anthony Taylor Kuchezesha Liverpool Vs Man Utd