Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia waandishi wa habari jijini Kigali kwamba wanachotaka ni ushindi dhidi ya APR.

Pluijm raia wa Uholanzi, yuko mjini Kigali kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda, utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Amahoro.

“Tunataka kushinda na hicho ndicho kilichotuleta. Lakini tunajua APR ni timu nzuri, tunaheshimu hilo. Lakini hakika tunataka kutengeneza mazingira bora ya mechi ya marudiano kule Dar es Salaam.

“Kushinda huku (Kigali), kutafanya tuwe katika nafasi nzuri ya kufanya vema zaidi,” alisema Pluijm.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchini Malawi ambapo Duncan Lengani atapuliza filimbi, wakati washika vibendera watakuwa Clemence Kanduku na Jonizio Luwizi.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Dar es Salaam, kwa usimamizi wa waamuzi kutoka visiwa vya Shelisheli, katikati Bernard Camille na pemebeni watakuwapo Eldrick Adelaide na Gerard Pool.

Allan Wanga: Nitawafunga Bidvest Wits
Kocha Wa APR Atamba Kuwaadabisha Yanga Kesho