Muongozaji mahiri wa video za muziki nchini Hanscana ametoa somo kwa wasanii wa muziki wa bongo fleva kuhusu kile anachodai kuwa ni mkanganyiko wa uelewa kwa wasanii, akilitaja kundi la wasanii wa kuimba kama sehemu ya changamoto iliyomfanya kutoa somo hilo.

Ni kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story), ambapo Hanscana amesema kuwa imekuwepo kasumba ya wasanii wengi kuwekeza pesa nyingi na nguvu zao katika kutayarisha video za nyimbo zao kwa ubora wa viwango vya kimataifa bila ya kuzingatia ubora wa maudhui yaliyobebwa ndani ya nyimbo hizo.

Katika kulitolea ufafanuzi suala hilo, Hancana amewataja wasanii wa miondoko ya kufokafoka (Hip hop) kama mfano wa kutazamwa kwa upande fulani, kwa kuwa ni kwenye kundi la wasanii wanaoongoza kwa nyimbo zenye maudhui bora na yenye kuwavutia wengi kwenye upande wa audio licha ya kuwa video zao mara zote huwa zenye ubora wa kawadia, na kwamba wasanii wa kuimba nchini wao huwekeza nguvu zao kwenye video nzuri bila kujali uzuri na ubora wa audio hasa maudhui yaliyo ndani ya nyimbo hizo.

“Mara chache sana kukuta wimbo wa rap ukasifiwa kwa video au kuwa na video kali, mara zote watasifu Lyrics, Beat, content na flows, lakini mara zote ngoma za waimbaji point yao kubwa ya kusogeza kazi zao ni music videos zao, ndio maana inafika kipindi wanasafiri mataifa ya mbali kufuata video not audio”

“Means they depend more kwenye video not content zao lakini kwa uelewa wangu mdogo, muziki ni audio not video, video is just a promotion material, so waimbaji jitahidini kuweka nguvu kwenye audio, wekeni nguvu kwa producers ili huku kwenye videos tuisitumie nguvu kubwa kuthibitisha ubora wenu.

Wazeni tu ngoma nyingi zilizofanya vizuri, hazikuwa na videos nzuri na nyingine hazikuwa na videos kabisa hii yote inathibitish muziki mzuir ni Audio”. amesema Hanscana.

Hii si mara ya kwanza kwa muongozaji huyo nyota nchini kushiriki maoni yake kuhusu mwendendo wa tasnia ya muziki, hasa katika mlengo wa kushauri namna nzuri ambayo wasanii wanawezakuitumia na ikawa yenye mchango mkubwa kwenye kazi zao za sanaa.

Harmonize afunguka siri nzito, Burna Boy na Davido

Changamoto za watoto wanazijua watoto wenyewe: Diwani
Utaratibu kuingia Stendi ya Magufuli wabadilika