Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC Zacharia Hanspope amezushiwa tena kujiuzulu nafasi hiyo.

Taarifa hizo zilionekana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku wasambazaji wakionyesha ushahidi wa kipande cha habari yenyewe iliyoambatana na picha kutoka kwenye blog ambayo haikufahamika mara moja.

Miaka miwili iliyopita wakati timu hiyo ikiongozwa na Ismail Aden Rage uvumi kama huo ulisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Tayari Hanspope mwenyewe amekanusha tena uvumi huo na kupuuza wale waliosambaza.

Comments

comments