Baada ya miaka 26 kupita ikiwa kama kumbukumbu ya mauaji ya vijana yaliyofanyika Soweto Afrika kusini waliouawa wakati wakitekeleza haki yao ya kikatiba ya kujieleza leo Jukwaa la katiba limeamka na kutaka mchakato wa kukamilisha katiba mpya uendelee.

Ikiwa ni muda mrefu umepita tangu mchakato wa kupata katiba mpya ulipo kwama wakati wa  kupiga kura ya kupitisha katiba pendekezwa Jukwaa la katiba tanzania (JUKATA) limeitaka serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kutangaza upya kwa mchakato wa katiba mpya.

Jukata limefikia uamuzi huo baada ya kuona serikali hii ya awamu ya tano haina dalili ya kushughulikiwa swala la upatikanaji wa katiba mpya pia kutokuona bajeti mawasilisho ya wizara ya katiba na sheria kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya.

Mwenyekiti wa bodi jukwaa la katiba  Deus .M. Kibamba amesema kuendelea kukaa kimya kwa serikali kuhusu Katiba mpya kunainyima fursa Tanzania kujenga demokrasia ya kweli inayoheshimu mgawanyo wa madaraka katika mihimili mikuu ya dola.

Deus Kibamba (1)

Aidha JUKATA imeitaka  Wizara ya katiba na sheria kupeleka  miswada ya marekebisho ya sheria zinazosimamia mchakato wa katiba mpya sambamba na vifungu vilivyopitwa na wakati ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro zilizojitokeza wakati wa mchakato ikiwepo ile ya kuirejesha tume kuwa kama chombo cha kitaalamu na mshauri kwenye mchakato.

Amesema kuwa kutokamilika kwa mchakato wa katiba mpya ni kinyume cha wito wa matumizi bora ya fedha unaosisitizwa na Rais John Magufuli pamoja na kuipongeza serikali ya hapa kazi tu ameitaka  kugeuka na kuiangalia suala la katiba.

 

 

Video: "tumepata mtoto nitampa jina la Tulia" - Mbunge Ulega
CAF Yawakubali Wachezaji Wote Wa Young Africans