Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametangaza na kutoa agizo kwa viongozi wa Halmshauri ya Kinondoni kuanza kutoa mikopo ya vitendea kazi kwa vijana mbalimbali wilayani huo zikiwemo Pikipiki ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi,

“Vijana wanaotaka kukopa Pikipiki waje, waje wajiorodheshe wakopeshwe Pikipiki walete rejesho serikalini tuna Billioni 1 imekaa tuu pale eti tunasubiri vijana waje, watakuja lini? Sasa nataka kuona vijana wananufaika na fedha hizo wajikwamue ili familia zao nazo zinufaike,”amesema Hapi

Aidha ameongeza kuwa dhana za kufanyia kazi ameshazifanyia kazi za kumwambia Mkurugenzi jambo hilo walifanye. Naibu Meya kama wakijitokeza vijana 400 Kinondoni watakaokopeshwa Pikipiki anataka kuhakikishiwa ndani ya muda mfupi fedha zile zinarudi, mpe mtu Pikipiki chukua kadi itunze yeye analeta ndani marejesho kila wiki unauhakika.

Jukata kufungua kesi dhidi ya katazo la maandamano

Baraza la Usalama lagawanyika
Video: Rais Magufuli asifu mchango wa Kingunge, Lissu alivyopaa dk 500 Ulaya