Mkuu wa Mkoa wa Iringa,  Ally Hapi, amegoma kuzindua jengo la kliniki katika lituo cha afya cha Mgololo kilichopo Kata ya Makungu Tarafa ya Kasanga.

Hapi amegomea uzinduzi huo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Mkoa wa Iringa ya Tarafa Kwa Tarafa ambapo ametembelea Tarafa ya Kasanga ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Aidha, baada ya kufika muda wa kuzindua Mkuu huyo wa Mkoa aligoma kwa kile alichodai ni kuwepo kwa harufu ya rushwa kutokana na kiasi cha fedha kilichotumika kwenye mradi kuwa tofauti na muonekano wa jengo lenyewe.

Hata hivyo, Hapi amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo, (TBA), Mkoani humo,  kuandaa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo ili ajiridhishe na baada ya kujiridhisha atarudi kuzindua au hatua nyingine zitachukuliwa endapo itabainika kuna ubadhirifu.

Mchezo wa Madagascar Vs Senegal waacha majonzi
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 10, 2018