Aliyekuwa rais wa Cuba, Hayati Fidel Castro(1926-2016) akiwa na mwenyeji wake  Hayati Mwalimu Julius Nyerere(1922-1999) Ruvu, Tanzania mwaka 1977 alipotembelea Tanzania Machi 17, 1977.

nyerere_castro

Fidel Castro ni kati ya watu wachache duniani waliojitabiria kifo kwani Novemba 25, 2016 aliwaaga wajumbe wa chama cha Kikomunisti cha Cuba kwa kuwaambia kuwa atakufa siku si nyingi hivyo amewataka waendelee kuenzi mapinduzi, na siku moja baada ya kutoa kauli hiyo akafariki.

Fidel Castro;

fidel-castro-obituary-slide-hton-master675

  • 1926: Azaliwa mkoa wa kaskazini mashariki wa Oriente nchiniCuba
  • 1953: Afungwa jela baada ya kuongoza maasi ambayo hayakufanikiwa dhidi ya utawala wa Batista
  • 1955: Aachiliwa huru kutoka jela chini ya mkataba wa msamaha
  • 1956: Akiwa na Che Guevara, aanza vita vya kuvizia dhidi ya serikali
  • 1959: Amshinda Batista, na kuapishwa waziri mkuu wa Cuba
  • 1961: Awashinda wapiganaji waliofadhiliwa na CIA waliovamia Bay of Pigs
  • 1962: Atifua mzozo wa makombora wa Cuba kwa kukubali USSR iweke makombora Cuba
  • 1976: Achaguliwa rais na bunge la Cuba
  • 1992: Aafikiana na Marekani kuhusu wakimbizi wa Cuba
  • 2008: Ang’atuka madarakani kwa sababu za kiafya
  • 2016: Afariki dunia

Mpina aipongeza singida kwa usafi
Gavana BoT: Hakuna Ubaya kuweka fedha kwenye ‘Fixed Deposit Account’