Sheikh Abeid Amani Karume ndiye Rais wa kwanza kuiongoza Zanzibar baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akiitawala hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.

Tangu hapo, baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere, muungano wa nchi hizi mbili ukazaa Tanzania na Karume akawa makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu 1964 hadi 1972

Nyerere na Karume wakichanganya udongo wa Tanganyika na Zainzibar kama ishara ya muungano wa nchi hizo mbili

Nyerere na Karume wakichanganya udongo wa Tanganyika na Zainzibar kama ishara ya muungano wa nchi hizo mbili

Abeid Karume alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili, 1972 kwa kupigwa risasi.

Mtoto wake, Amani Abeid Karume alifuata nyayo za baba yake na kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar tangu mwaka 2000 hadi 2010.

Vyuo 22 vyaitunishia misuli TCU
Gambo ataka busara itumike utekelezaji agizo la Waziri Mkuu