Fuvu la kichwa cha aliyekuwa chifu na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898) lilirudishwa Tanganyika tarehe 9 Julai 1954 na kuhifadhiwa katika jengo la makumbusho ya Mkwawa kwenye kijiji cha Kalenga.

Kichwa cha Chifu Mkwawa inasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen.

Baada ya Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Wajerumani walikataa habari za fuvu hili na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kulipata.

Baada ya vita vikuu ya pili, Ujerumani pia ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza, Gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Ujerumani ilikuwa na mafuvu 2000, 84 yaliyokuwa na namba zilizionyesha yalitokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Gavana Twining wa Tanganyika aliyapanga kufuatana na ukubwa na kutazama yale yaliyokuwa na vipimo vya karibu na ndugu wa Mkwawa aliowahi kuwapima kabla ya safari yake. Ndipo aliteua fuvu lenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.

Lowassa aingia mikononi mwa polisi Geita, wamhoji ‘kimjadala’
Mbarawa azitaka taasisi kujiunga na kituo cha kumbukumbu IDC