Wasandawe ni kabila la pekee lenye viini nasaba(kizazi) vya zamani kuliko makabila yote Duniani.

Wasandawe wanaishi hasa katika eneo la wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma, katika tarafa mbili, yaani Farkwa na Kwamtoro.

Lugha yao ni Kisandawe, asili ya Kikhoisan, ina fonimu nyingi kuliko lugha zote duniani, zikiwa ni pamoja na “click sounds”. Kisandawe ni lugha inayotajwa kuwa ya zamani kuliko zote, kwa kuwa inafanana bado na zile za wenzao wa Kusini mwa Afrika(Bushmen), ingawa walitengana miaka 40,000 iliyopita.

Baada ya Serikali kuanzisha shule za kata kama Farkwa Secondari, Kwamtoro Secondari, Makarongo Secondari, Gwandi Secondari, Kurio Secondari na nyingine nyingi, Wasandawe sasa wanawasomesha watoto wao kwani katika miaka ya nyuma wengi wao walikuwa hawajasoma, pia wameanza kujihusisha na kilimo japo bado wanaendelea na uwindaji.

Video: Manispaa ya Ilala kuondoa mabango yasiyolipiwa
Serikali yajipanga kuhakikisha hali ya chakula ni nzuri nchini

Comments

comments