Wakilindi ni Wasambaa wenye asili ya Kiarabu, na chanzo cha kuwa Wasambaa ni kiongozi aliyeitwa Mwene/Mfalme Mbegha (Mbega).

Wasambaa ni wakazi wa milima ya Usambara katika Tanzania kaskazini-magharibi.

Na Mbegha ni jina la mtu muhimu katika historia ya Wasambaa anayekumbukwa kama mfalme wao au mwene mkuu wa kwanza katika kundi hili. Familia ya watawala iliyoanzishwa naye hujulikana pia kama nasaba ya Kilindi.

Mbegha kiasili alikuwa mtoto wa Mwarabu aliyetoka Pemba na kuhamia Kilindi na mke wake Mngulu. Mbegha alikuwa mtoto kigego aliyewahi kupata meno ya juu hali iliyo onekana kama ishara baya kati ya makabila mbalimbali na mara nyingi waliuawa.

Kutokana na tabia ya kuuliwa watoto wanaowahi kuota meno, Mbegha yeye alifanikiwa kuishi lakini baada ya kifo cha wazazi na kakaye alinyimwa urithi wake na nduguye waliomkumbuka kama kigego na kumshtaki kuwa ni mchawi.

Mbegha alihamia Kilindi, kutokana na umaarufu wake kama mwindaji, Chifu wa Kilindi akampatia nyumba akawa rafiki wa mtoto wa chifu. Siku moja walipoenda pamoja kuwinda huyu kijana aliuawa na nguruwe mwitu na Mbegha aliona hawezi kurudi Kilindi akiogopa hasira ya chifu akaamua kuhama akiwa pamoja na vijana 14 na mbwa zake.

Walienda hadi huko Zirai kando la Usambara. Hapo wazee wa Bumbuli wakamkaribisha Mbegha na chifu Mbogho alimpa binti yake kama mke akampandisha kuwa chifu pamoja naye.

Sifa za Mbegha zilisambaa kwa Wasambaa wote. Wakati ule Wasambaa wa Vuga walikuwa na vita dhidi ya Wapare wakaona wapate usaidizi wa Mbegha. Kiongozi wa Vuga akamwomba Mbegha ahamia kwao na kuwa Mwene wao.

Ndipo Mbegha akahamia Vuga pamoja na mke ambapo alikaribishwa kwa mapigo ya ngoma kubwa, Watu wa Vuga wakamjengea nyumba.

Mke wa Mbegha alijifungua mtoto aliyezaliwa kwenye kitanda kilichofunikwa kwa ngozi ya simba aliyomahi kuua Mbegha wakati akielekea Vuga. Mtoto aliyezaliwa juu ya ngozi ya simba akaitwa Simba, akawa mrithi wa Mbegha ndipo akipewa pia jina rasmi la Buge (Bughe).

Kutokana na jina la Buge watawala wa Vuga waliendelea kutumia cheo cha Simba Mwene. Baadaye alikuwa chifu wa Bumbuli kwa kibali cha baba.

Mbegha aliendelea kuoa mabinti kutoka koo za Wasambaa mbalimbali na kuweka wanawe kama watawala na wawakilishi wake juu ya vijiji vya mama zao. Kwa njia hii aliunganisha Usambara na koo za Wasambaa na kuweka msingi kwa utawala wa kifalme katika Usambara uliosimamia sehemu kubwa ya Tanzania ya kaskazini kabla ya kuja kwa Wazungu. Watawala wa nasaba yake waliomfuata Vuga waliendelea kuoa wake wengi na kuweka wana wao kama watawala wadogo mahali pa mama.

Baadaye mzee Mbegha alikaa pamoja na wazee 5 pekee waliomtunza hadi alipoaga dunia kufuatia kuugua kwa siku tatu.

Wazee waliomuuguza Mbegha hawakutangaza kifo chake waliendelea kuandaa mazishi na ufuasi wake kimyakimya. Walituma ujumbe kwa Buge – Simba aje haraka babake ni mgonjwa. Buga alipofika alitangazwa mara moja kuwa mwene mpya.

Mbegha alizikwa katika kaburi ndani ya ngozi ya ng’ombe dume mweusi pamoja na paka mweusi.

Video: Makonda ataja watuhumiwa biashara ya Madawa ya Kulevya, wapo Polisi, wasanii maarufu
Goncalo Guedes: Umri Wangu Ulikua Kikwazo Kutua Old Trafford