Wapangwa ni kabila linalopatikana nchini Tanzania katika pwani ya mashariki ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe.

Wapangwa lugha yao ni Kipangwa na mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa na hufumwa.

Pia hujenga nyumba zao za asili kwa kutumia miti asili kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu japo kwa sasa wanajenga yumba zao kwa matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati kama ilivyo kwa makabila mengi kupoteza asili zao kutokana na teknolojia ya sasa.

Wapangwa ni wabunifu kwani hata usafiri wao wa asili wametengeneza chombo kiitwacho Ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.

Pia Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na uwindaji wa wanyama pori kama vile (kwa lugha yao) Videke, Nyhaluchi, Ng’ese, Mahtu Ngwehe, na Ng’wali.

Chakula chao ni kikubwa ni ugali wa mahindi, ulezi na kitoweo chao ni maharage, samaki, nyama, jamii ya mboga mboga na matunda ya asili kama vile; masada, savula, makuhu, mahofita,mafudo, minhingi, vudong’o na nisongwa.

Kinywaji chao ni pombe (Ukhimbi) yaani kangala, komoni, ulanzi ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi.

Wapangwa wanalima mazao mbalimbali ya chakula katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito. Pia hulima mazao ya biashara kama kahawa, chai, pareto, mahindi na njia ya ulimaji wao ni ya ushirika wenyewe huita ‘Njhiika’.

 

 

Niyonzima anena kuelekea pambano lao dhidi ya Azam FC
Video: HipHop 6 mpya na kali