Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameitaka  wizara ya maliasili na utalii kuwatumia wasanii hapa nchini katika kutangaza utalii na vivutio vilivyopo hapa nchini.

Mh. Hapi amesema kuwa wasanii wanauwezo mkubwa kutangaza vivutio vya nchi kutokana na ukubwa wa majina yao na kuingizia taifa mapato makubwa pia kuboresha maisha yao wenyewe, huku akiwasisistiza wasanii hao kuifanya kwa uadilifu pindi watakapopatiwa kazi hizo

Jana akizungumza na wasanii wa muziki pamoja na filamu Ndg Hapi aliwataka wasanii kutumia ukubwa wa majina yao katika mitandao ya kijamii kwa kufanya biashara huku akiazimia kuhakikisha anawatafutia wasanii hao mwalimu wa kufundisha elimu ya ujasiriamali ambapo amesema elimu hiyo itawasaidia matumizi sahihi ya pesa.

Katika Mazungumzo hayo Hapi amewataka pia wasanii kujishughulisha na biashara mbalimbali pia  ikiwepo kununua hisa kwenye makampuni mbalimbali pamoja na kuchukua mikopo katika mabenki  baada ya kupata elimu ya ujasiriamali ili kuondokana na hali ngumu za kimaisha huku akiongeza kwamba wasanii wa Tanzania wanaishi maisha ya kimasikini tofauti na wasanii wa nje.

Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nickson Simon ‘Niki II’ ameeleza kuwa changamoto za kazi ya sanaa hapa nchini haziwawezeshi wasanii kufikia malengo yao na kwamba Wasanii wengi wanaishi maisha ya tabu tofauti na ukubwa wa majina yao.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds media group Ruge Mutahaba amewasisitizia wasanii kuzichukua na kuzitumia fursa zilizotajwa na Mkuu wa wilaya zikiwemo za kutumia mitandao ya kijamii kwa faida.

 

 

 

Coke Aondoka Sevilla CF
Video: Aje ya Ali Kiba yafanyiwa 'remix' Kenya