Hitmaker huyo wa Matatizo, amekiambia kipindi cha Fiday Night Live cha EATV kuwa ndani ya lebo yao hawajawahi kushindana wala wanapotoa nyimbo hawatoi kwa mashindano kati yao ila mashabiki ndio wanaowachukulia hivyo lakini kibiashara kwao inakuwa vizuri.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio yakwao wote.

Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kudai kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake wa kuachia nyimbo zao.

Talaka na Gadner ni moja ya mambo Jide anamshukuru Mungu 2016
Nnape akiri kuwepo udhaifu ''BASATA''