Msanii wa muziki wa bongo fleva na CEO wa lebo ya muziki ya Konde Gang Rajab Abdul maarufu Harmonize amemtangaza rasmi msanii wa Hip hop Ibrahim Mandingo maarufu kama Country Boy kwamba amejiunga na kundi hilo.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari Harmonize amewazawadia wasanii wake ambao wapo katika lebo ya Konde Gang kila mmoja gari aina ya Crown.

Itakumbukwa mapema wiki hii kundi hilo liliwatambulisha wasanii Ally Killy Omary maarufu kama Killy na Rashid maarufu kama Cheed waliotoka katika kundi la muziki lililo chini ya msanii maarufu Alikiba, Kings Music, ambapo usiku wa leo septemba 11, 2020 kutakuwa na ‘show’ itakayo fanyika makao makuu ya Konde Gang. 

Kwa sasa kundi hilo lina jumla ya wasanii sita ambao ni Harmonize, Ibraah, Young Skales, Killy, Cheed pamoja na Country Boy.

Ujerumani,Urusi kushirikiana uchunguzi sakata la Navalny
Uganda kufungua anga rasmi