Mwanamuziki kutoka label ya WCB, Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Sina, ameweka wazi kuwa bado anaishi kwenye nyumba ya kupanga huku shughuli za ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa ukiendelea.

Amesema kuwa ni nyumba ambayo imemgharimu kiasi kikubwa cha pesa na hayupo tayari kuweka wazi ni kiasi gani cha fedha amegharimu ila anategemea mwisho wa mwaka huu mjengo utakuwa umekamilika.

Aidha ameeleza kuwa fedha anayoipata katika show za muziki ni hela ambayo haiwezi kutosha kukamilisha jengo hilo, hivyo imembidi ajiongeze na kujishughulisha na shughuli nyingine ili kuongeza kipato cha kumalizia jengo hilo.

“flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi, Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,” amesema Harmonize.

Hii ihamasishe vijana ambao hawana mpango wa kujenga makazi yao, Harmonize amekuwa mfano mzuri sana katika kujifunza maisha na kuishi bila kukata tamaa, historia yake infahamika alianzia bongo star search, hadi sasa kuwa  mwanamuziki bora anayefanya vizuri Tanzania na nje ya nchi chini ya lebo kubwa WCB.

Mbowe amkumbuka Kikwete, asema hali kwa sasa ni tete
LIVE BREAKING: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu Kenya