Mwanamuziki Harmonize bado yuko katika kufuatilia sakata la madai ya stahiki zake akiishutumu kampuni ya usambazaji muziki nchini Ziiki kuwa haijawahi kumpatia mauzo ya kazi zake kwa kipindi kirefu kinyume cha utaratibu.

Nyota huyo amedai kuwa hajawahi kunufaika kwa namna yeyote ambapo amedai kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakichukua pesa zote kwenye platform hiyo.

Harmonize ameitaja kampuni ya Ziiki pamoja na Wasafi kuhusika na suala hilo huku akidokeza kuwa anahitaji wanasheria wasiopungua watano ili kulishughulikia suala hilo kisheria kwa kile alichodai kuwa makampuni hayo ni kama yameungana kuyachezea maisha yake.

“Ubaya unaanza pale mtu unapotaka jasho lako ili usisaidie familia yako kama wao wanavyofanya” ameandika Harmonize

Huku akituma ujumbe wa wazi kwa Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, punde baada ya kuteuliwa kuhodhi nafasi hiyo aanze kwa kulishughulikia suala hilo ili aweze kupata haki yake.

“Kaka mkubwa hongera na nakuomba uanze na hili, mama anajua kabisa wewe ni Suluhu nyingine.” Ameongeza

Pamoja na yote hayo, kwenye ujumbe huo aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Konde boy ameweka wazi kuwa hakuwahi kukusanya mapato yake yanayotokana na mauzo ya kazi zake za sanaa, na kwamba punde baada ya kuliweka suala hilo hadharani amepokea simu kutoka kwa mmoja wa watu wa kampuni ya Ziiki akimuomba wampatie kiasi cha pesa ili suala hilo liishie njiani

Harmonize amedhihirisha kutoridhishwa na jambo hilo kiasi cha kubainisha kuwa wakati wa mazungumzo na muwakilishi huyo wa Ziiki alirekodi mazungumzo hayo kama sehemu ya ushahidi wa suala hilo ambalo punde litafikishwa mikononi mwa sheria.

Harmonize afunguka siri nzito, Burna Boy na Davido

Kocha Robertinho akubali tatizo Simba SC
Tarimba aibuka tena sakata la mkataba Young Africans