Baada ya kufanikiwa kumuweka mkongwe Juma Nature kwenye ‘Kiboko ya Mabishoo’, Harmorapa amerudi na CPwaa kwenye ngoma nyingine mpya aliyoipa jina la ‘Nundu’.

Rapa huyo ambaye alifanikiwa kuweka kishindo kizito kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii tangu alipoachia wimbo wake rasmi wa kwanza, amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kuipokea ‘Nundu’.

“Coming soon kaa tayari kwa kuipokea ngoma mpya #Nunduloading @ivual @majani187 @SGSsabukamusic,” ameandika kwenye Instagram.

Nundu ina kila dalili za kuwa wimbo mkubwa kutokana na jinsi ilivyowakusanya watayarishaji wakali huku mkono wa ‘super duper producer’ P-Funk Majani ukihusika kuweka mambo sawa kwa kufanya ‘mixing na mastering’.

Wimbo umepikwa ndani ya studio za Bongo Records ya Majani na mtayarishaji Lufa ndiye aliyehusika kwa hatua zote za mwanzo.

Serikali yapigilia msumari wa moto kuhusu mwenge
Wakili Akabiliwa na Kifungo Cha Miaka 150 Jela Kwa Kumkashfu ‘Mfalme’