Harmorapa amejikuta katika hali ya mtetemo baada ya kufanikisha sehemu ya ndoto yake ya kukutana na Wema Sepetu na kumuonesha hadharani jinsi anavyompenda.

Rapa huyo alimpa mshangao Wema alipoenda kumpongeza katika hafla ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday Gala) iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, akiwa ameshikilia ua huku mkono wake ukiwa umefungwa ‘mhogo’ mithili ya majeruhi aliyetoroka hospitalini.

“Huyu si ni Harmorapa… jamani,” Wema alisema kwa mshangao baada ya kumuona Harmo ghafla mbele yake. Bila kupoteza sekunde, rapa huyo alipiga goti na kumkabidhi Tanzanian Sweetheart ua jekundu kama ishara ya upendo.

Wema aliyempa kumbato Harmokiki na kumkabidhi kikuza sauti ili aseme japo neno, alisema kuwa anamuona Harmo akiwa anatetemeka hivyo alimtaka atulie ili ‘afunguke’.

“Jamani nimefurahi sana kumuona Wema, nimetoka hospitali kwa ajili yake, yaani ni upendo ulioje,” alisema Harmorapa

“Usitetemeke, ongea vizuri…anatetemeka jamani” alisikika wema aliyemuwekea mkono begani.

“[Natetemeka kwa sababu] ni mapenzi jamani siamini,” alisema Harmorapa kabla ya kuendelea na lisala yake aliyoitoa kama mtindo-huru mbele ya umati.

Harmorapa aliwahi kuweka wazi mwaka jana kuwa anampenda Wema Sepetu na kwamba ni mwanamke wa ndoto yake.

 Hata hivyo, wakati huo Wema alionesha kutozipenda kauli alizozitoa Harmo kwa siku kadhaa mfululizo kwa kuzingatia kuwa yeye ni dada mkubwa kwa msanii huyo.

It’s all good. Jana Harmo alifanikisha sehemu ya ndoto yake kuwa uso kwa moja na Wema na hata kupata kumbato (hug); huku ua lake likipokewa mbele ya umati! Dada kampa furaha mdogo wake.

Akaunti milioni 50 za Facebook zadukuliwa, yammiliki pia
'Nahodha wa MV Nyerere hakuwa na vigezo'

Comments

comments