Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Kenya Harrison Mwendwa ameripotiwa kuwasili jijini Dar es salaam mapema leo Ijumaa (Juni 24), tayari kwa kukamilisha taratibu za usajili.

Mwendwa anahusihwa kwenye mipango ya usajili wa klabu ya Simba SC, ambayo imedhamiria kuwa na kikosi bora na imara msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kimataifa msimu ujao 2022/23.

Taarifa zinaeleza kuwa, baada ya kuwasili Dar es salaam, kiungo huyo alipokewa na viongozi wa Simba SC, na mchana huu anatarajiwa kukamilisha sehemu ya mazungumzo, kisha atasaini mkataba.

Mwendwa aliwahi kuhusishwa na Simba SC wakati wa Dirisha Dogo la usajili msimu huu, lakini mpango huo ulishindakana kutokana na mkataba uliokuwepo kati yake na klabu ya Kabwe Warriors ya Zambia.

Hadi sasa Simba SC imeshamtambulisha Mshambuliaji Moses Phiri kutoka Zambia, huku ikitangaza kuachana na Kiungo Rally Bwalya na Beki Serge Pascal Wawa, ambao wameangwa rasmi katika michezo ya Ligi Kuu dhidi ya KMC FC na Mtibwa Sugar.

Makumbusho ya wapigania Uhuru nchini kuboreshwa
Matola afichua siri kiwango cha Banda, Sakho