Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amethibitisha kuwa Nahodha, Harry Kane atacheza katika mchezo wa leo dhidi ya Marekani.

Kocha huyo aliingiwa na wasiwasi wa kushindwa kumtumia Mshambuliaji huyo, katika mchezo huo kufuatia majeraha alioyapata katika mchezo wa Kwanza wa Kundi B dhidi ya Iran ambao walikubali kichapo cha 6-2.

Akiwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo huo, Kocha Saothgate alisema: “Harry yupo vizuri. ulikua uamuzi wa kijasiri kumwacha nje ya kikosi cha kwanza tulipocheza na Iran!”

Kocha huyo alilazimika kutoa taarifa hizo, baada ya Mlinda Lango wa England, Jordan Pickford kukiri Kane alifanya mazoezi na wachezaji wengine juzi Jumatano.

England inayoongoza Msimamo wa Kundi B, leo Ijumaa (Novemba 25) itacheza dhidi ya Marekani katika mchezo wa Pili wa Kundi hilo, katika Uwanja wa Al Bayt.

ICC kuthibitisha mashtaka dhidi ya Kony
Simba SC kusajili watatu dirisha dogo