Mshambuliaji Harry Kane atakosekana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya England dhidi ya Uswiz utakaochezwa baadae hii leo, kwenye uwanja wa King Power mjini Leicester.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa mapema hii leo na kituo cha televisheni cha Sky Sports, kocha mkuu wa England, Gareth Southgate amedhamiria kumpumzisha mshambuliaji huyo wa klabu ya Tottenham, na jukumu la unahodha atalikabidhi kwa beki Eric Dier.

Kane alicheza dakika 573 wakati wa fainali za kombe la dunia na kufunga mabao sita, na tangu mwanzoni mwa msimu uliopita amecheza michezo 61 ya klabu yake na timu ya taifa.

“Harry ni sehemu ya wachezaji wa kuigwa katika kikosi cha England, kutokana na mazuri anayoyafanya kila anapopata nafasi, kucheza ama kutocheza katika mchezo wa kesho (Leo) itategemea na maamuzi nitakayo yachukua,” amesema.

“Itapendeza kama atapumzika na kuwaangalia wenzake wakicheza ili ajifunze kupitia mchezo dhidi ya Uswiz, lakini bado ninasisitiza suala la kucheza ama kutokucheza litategemea na maamuzi yangu ya mwisho,” ameongeza.

“Tumezungumza na Harry mambo kadhaa na tumekubaliana kuhusu maamuzi yatakayotokea, hivyo ninawasihi waandishi wa habari kuendelea kuwa na subira, na mtaona kabla ya mchezo kama mchezaji huyu anaweza kuwa sehemu ya kikosi ama ala.”

Kwa mujibu wa Sky Sports, kikosi cha England kinatarajiwa kupangwa hivi: Jack Butland, James Tarkowski, Danny Rose, Kyle Walker, Trent Alexander-Arnold, Fabian Delph, Ruben Loftus-Cheek and Danny Welbeck.

Museveni azionya nchi za Magharibi na siasa yao, ‘kaeni mbali’
Mbaroni kwa kuweka video mtandaoni akilishwa na mwanamke