Wachezaji Kevin Yondani, Feisal Salum, Meddie Kagere na Amis Tambwe wametajwa kuwa bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kufuatia kucheza sanjari na kiungo Haruna Niyonzima.

Kiungo huyo aliemaliza mkataba wake Young Africans na kuagwa kwa heshima, amewataja wachezaji hao kuwa bora kwa mapendekezo yake kutokana na umahiri walionao wakiwa dimbani.

Amesema tangu alipoanza kucheza soka katika Ligi Kuu Tanzania Bara hadi anaondoka Young Africans msimu wa 2020/21, hakuwahi kuona wachezaji wenye umahiri na kuipenda kazi yao kama hao aliowataja.

“Kwa upande wa mabeki namkubali sana Yondani, Viungo nampenda sana Feisal Salum ila kwa washambuliaji Meddie Kagere ni hatari”

“Tambwe pia nampenda kwa sababu nimecheza naye, Tambwe akisimama mbele unajua alama tatu zinapatikana tu kwa magoli yake ya kichwa.”

“Kwa mapenzi yangu binafsi wachezaji hawa ndio bora kwangu na nitaendelea kuwapa heshima kwa walichokifanya katika muda wote niliocheza hapa Tanzania.” amesema Niyonzima.

Lamine Moro kuondoka kiroho safi
Klabu bingwa CECAFA yaahirishwa