Kampuni ya Emirates Aluminium ACP imemkabidhi Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Hassan Dilunga Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu hiyo.

Dilunga alipigiwa kura na Mashabiki wa Simba SC kwa njia ya Mtandao na kuwazidi wachezaji wenzake Sadio Kanoute na Rally Bwalya, baada ya kushindwanishwa kwa mwezi Oktoba.

Kwa mwezi Oktoba, Dilunga amekuwa ni chaguo la kwanza kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, huku pia akianza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika waliopoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy, jijini Dar es salaam.

Hata hivyo pamoja na kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo hiyo, Dilunga hakuwa na bahati ya kucheza kwa dakika zote 90 kwenye michezo ambayo alianzishwa kwenye kikosi cha kwanza msimu huu 2021/22.

Katika viungo hao watatu walioingia fainali ni mmoja tu alifanikiwa kutupia alikuwa ni Bwalya ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy pamoja na ule mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mfumo wa malipo ya maegesho kuanza rasmi Desemba mosi
Fiston Mayele amfanyia kauzibe Makambo Young Africans