Kiungo Mshambuliaji Hassan Dilunga amethibitisha anaendelea kujiuguza vizuri na huenda akaonekana tena Dimbani mwezi Januari mwaka 2023.

Dilunga alishika Vichwa vya Habari katika Vyombo vya Habari Tanzania pamoja na Mitandao ya Kijamii, baada ya kuthibitika amechwa kwenye kikosi cha Simba SC kwa msimu ujao 2022/23.

Kiungo huyo amesema anaendelea vizuri na ana matarajia mkubwa ya kucheza tena soka kuanzia mwezi Januari mwaka 2023 kama mambo yatakwenda vizuri.

Katika hatua nyingine Mchezaji huyo Dilunga amesema Mkataba wake umeisha (Umebakiza siku chache) na bado hajasaini mkataba mpya na timu hiyo, lakini kuna Mabosi wa Simba Wamemtafuta kufanya mazungumzo.

“Upande wa afya yangu ninaendelea vizuri kwa sasa, ila kurudi tena Uwanjani kwa ajili ya kucheza mpira labda mwezi Januari mwaka ujao.”

“Nawashukuru viongozi wa Simba SC kuendelea kuwa karibu na mimi katika kipindi hiki kigumu kwangu, Mkataba wangu umekwisha kwa sabau umebakiza siku chache sana.”

“Baadhi ya viongozi wangu wamenifuata mara kadhaa kwa ajili ya mazungumzo, lakini siwezi kusema sana kuhusu hilo kwa sababu ambazo sitakuwa tayari kuzitaja hapa.” amesema Dilunga

Misimu minne iliyopita Dilunga alisajiliwa Simba SC akitokea Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro na kuwa sehemu ya kikosi kilichoipa mafanikio klabu huyo ya Msimbazi ndani na nje ya Tanzania.

Alipatwa na majeraha msimu uliopita, hali iliyopelekea kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Kenya: Raila Odinga anaongoza mbele ya William Ruto
Matumizi sarafu za kidigitali yapendekezwa