Kutokana na kile kinachoelezwa na wataalam wa makuzi na saikolojia kuwa mtoto hujifunza na kujaribu mambo mengi kutoka kwa wazazi wake, wazazi wametajwa kuwa chanzo cha wanafunzi wa shule ya msingi mkoani Kilimanjaro kulawitiana.

Hayo yamethibitika baada ya kufanyika uchunguzi na ufuatialiaji baada ya kuwepo malalamiko mengi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Kaloleni mkoani Kilimanjaro wamekuwa wakilawitiwa na wa kike kufanya mapenzi na watu wazima.

Gazeti la Mwananchi lilifanya mahojiano na wanafunzi hao, ambapo mwanafunzi mmoja alikiri kulawitiwa na mwenzake kwenye makaravati ya barabara.

Mwanafunzi huyo alipoulizwa alifahamu vipi mambo hayo ya ulawiti, alidai kuwa alijifunza kwa kuwaangalia wazazi wake wakifanya.

“Nilikuwa nawaona baba na mama wanafanya, ndio nikaamua kujaribu,” alisema mwanafunzi huyo. “Lakini toka tupelekwe polisi nimeacha kabisa huo mchezo,” aliongeza.

Akizungumzia kuhusu uwepo wa vitendo hivyo mashuleni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema kuwa walibaini uwepo wa suala hilo baada ya walimu kuwahoji kwa kina wanafunzi kwani maendeleo yao kitaaluma yalikuwa yakiporomoka.

Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo afanya ziara ya Kushtukiza
Walimu watoa siku 15 kwa Serikali kumaliza madai yao, ‘hatutaki lawama’