Siku chache baada ya kuelezwa kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Zika huambukizwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes, madaktari nchini Marekani wamebaini kuwa ugonjwa huo pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Madatari wa Jimbo la Texas katika kituo cha udhibiti wa maradhi kinachojulikana kama ‘Centers for Disease Control and Prevention’ wameeleza kubaini kuwepo kwa maambukizi ya ZIKA katika jimbo hilo, huku wao pamoja na maafisa wa Dallas wameeleza kuwa wamefuatilia na kubaini kuwa maambukizi ya ZIKA yanasambaa pia kwa njia ya kujamiiana.

Wataalam wameeleza kuwa wamebaini mtu mmoja katika jimbo hilo aliyeambukizwa virusi vya ZIKA bila kuumwa na mbu na wanaamini alipata virusi hivyo kwa kujamiiana na mpenzi wake aliyekuwa kusini mwa Marekani, ambaye pia alibainika kuwa na virusi hivyo.

Imeelezwa kuwa virusi vya ZIKA hubebwa kwenye manii na kumuambukiza mtu asiyekuwa navyo kwa njia ya kujamiiana.

Ugonjwa huo husababisha wanawake waja wazito kuzaa watoto wenye vichwa vidogo.

 

Mabingwa Watetezi Wanusurika Mbeya
Jumuiya ya Taasisi za Kiislam zapinga marudio ya uchaguzi Zanzibar