Watumiaji wa bidhaa za kampuni ya Marekani ya ‘Apple’ wamekubwa na hatari ya kudukuliwa taarifa zao na wezi wanaodaiwa kutumia program hatari ya kimtandao kufanya uhalifu huo, hususan nchini China.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa imenza kuchukua hatua za kukabiliana na uhalifu huo unaowalenga zaidi watumiaji wa simu za Iphone na iPad walioko nchini China huku ikieleza kuwa shambulio linalotekelezwa na wahalifu hao ni kubwa na halijawahi kuikumba kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na BBC, Apple wameeleza kuwa wadukuzi wamebuni namba za siri ambazo huwawezesha kutumia vifaa vya vya Apple kuingiza program zinazoathiri mawasiliano ya watumiaji wa bidhaa hizo kabla ya kudukua taarifa zao.

Kufuatia shambulizi hilo, Apple wamethibisha kuwa wameondoa vifaa vyao vyote katika mzunguko wa soko nchini China ambavyo vinatiliwa shaka ya kuvamiwa na wahalifu wa kimtandao nchini humo.

Zouma: Diego Costa Ni Muongo (Video)
Unachopaswa Kufanya Unapoandamwa Na Tatizo Zito