Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini(Chadema), Godbless Lema  ya kupinga kunyimwa dhamana inatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Arusha, Salma Maghimbi.

Lema alikamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma tangu wakati huo anashikiliwa kwenye Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56.

Aidha, baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha  katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikataa rufaa ya kupinga uamuzi wa Mahakama kumpa mbunge huyo wa Arusha.

Vilevile Desemba 20, mwaka huu Mahakama ilitoa siku 10 kwa mawakili wa Lema kuwasilisha maombi ya kukata rufaa hiyo baada ya kuwasilisha ombi la kuongezewa  muda hivyo, hata hivyo waliwasilisha muda huo huo.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Arusha, Modesta Opiyo aliyetoa uamuzi wa ombi hilo amesema hana sababu ya kuzuia kuongezwa muda wa kukataa rufaa.

Kampuni za simu nchini hatarini kufungiwa
Video: Majaliwa awasha moto, ataka jibu, Nyoka wa maajabu afa na mtu wake