Mahakama Kuu ya Tanzania, leo imetoa hukumu kuhusu namba 37 ya mwaka huu iliyofunguliwa na Peter Kibatala akiomba ufafanuzi kuhusu sheria ya namba 104 (1), kuhusu kukaa au kutokaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura.

Kupitia hukumu iliyotolewa baada ya kesi hiyo kusikilizwa siku tatu mfululizo na majaji watatu, mahakama imeamua kutoruhusu mikutano wala watu kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika Jumapili, Oktoba 25.

MITA 200

Kesi hiyo ilifunguliwa Oktoba 16 mwaka huu na wakili Peter Kibatala na ilipewa usajili namba 37 ya mwaka huu, akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri ya kifungu cha 104 (1) cha sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la, wananchi kukaa kwa utulivu mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo vyao.

Wakili Kibatala alifungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC).

Hii ndiyo hukumu iliyotolewa na mahakama:

pAGE 1pAGE 2pAGE 3

Agnes Masogange Ang’ang’ania Licha Ya Kukataliwa
Van Gaal Akiri Kuzidiwa Na Mzigo Old Trafford