Rapa wa Kenya, Octopizzo amepiga hatua kubwa ya muziki wake kwa kuionesha dunia kuwa muziki mzuri zaidi unapatikana pia Afrika Mashariki na unaweza kupendwa hata kuliko ule wa Beyonce.

Rapa huyo wa Kibera amevunja rekodi ya Afrika katika mtandao wa iTunes baada ya album yake ya LDPC (Long Distance Paper Chasers) kushika nafasi ya kwanza kwa umaarufu katika mtandao huo huku akiwafunika Dr. Dre na album yake mpya kubwa ya ‘Compton’ pamoja na Beyonce na album aliyoipa jina lake ‘Beyonce’.

Octopizzo-11

Hatua hiyo ni kubwa kuwahi kutokea kwa msanii yoyote wa Afrika anaefanya kazi ndani ya bara hili. Inaweza kumpa nafasi kubwa zaidi kwenye ulimwengu wa muziki kwa kuwa watu wengi zaidi duniani wataanza kumfuatilia kwa kuwa ameifunika Compton ambaye ndiyo album iliyozua gumzo zaidi kwa wiki hizi mbili.

CNN Wajishusha kwa Rais Kenyatta Baada Ya Kuwashukia
Irene Uwoya Apata Tiketi Ya Kuingia Bungeni, Sasa Ni Mheshimiwa