Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumatano Septemba 1, 2021 inatarajiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anayetaka imwachie huru kwa kuwa haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka ya ugaidi dhidi yake.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alikamatwa mwezi Julai jijini Mwanza pamoja na wanachama wengine 10 walipokuwa wakijiandaa kufanya kongamano la kushinikiza kupatikana kwa Katiba Mpya nchini.

Hatahivyo jana Agosti 31, 2021 kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji mbele ya Jaji Elinazer Luvanda, ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando aliieleza Mahakama kuwa walipokea pingamizi kutoka kwa mawakili wa Mbowe.

Wakili wa Mbowe na wenzake, Peter Kibatala aliieleza Mahakama hiyo kuwa wateja wake wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi namba 21 ya mwaka 2002, Mahakama hiyo imetengwa maalumu kwa ajili ya kusikiliza makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, hivyo inakosa mamlaka ya kusikiliza mashtaka ya ugaidi dhidi ya wateja wao.

Mbowe, anayekabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi na ugaidi, amekuwa rumande kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa akisubiri hatima yake.

Bocco aachwa Dar es salaam
Magori: Wamefungwa na vibonde