Hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupata wawakilishi wawili wa Bunge la Afrika Mashariki itajulikana mapema mwezi ujao.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah mara baada ya kutangaza upya siku ya kufanyika Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki kwa ajili ya wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Aidha, Uchaguzi huo wa Bunge ulifanyika April 4 mwaka huu ambapo wagombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipigiwa kura za hapana kwa kutotimiza masharti na vigezo vya uchaguzi huo.

“Uchaguzi wa wajumbe hao wawili watakao jumuika na wenzao saba waliochaguliwa kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika bunge la EALA utafanyika Mei 10, mwaka huu katika mkutano wa saba wa bunge unaoendelea mjini Dodoma,”amesema Dkt. Kashilillah.

Hata hivyo, Dkt. Kashilillah amekiasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kufuata masharti ya Uchaguzi huo yaliyoainishwa ili kuondoa mgongano usiokuwa na tija.

 

Mpina atoa neno kwa wakazi wa Morogoro
Prof. Kabudi awafunda watetezi wa Haki za Binadamu