Mahakama jijini Kigali inatarajia kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu kesi dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na Mama yake Adeline Rwigara.

Wawili hao wameshitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Kwa pamoja walikanusha madai hayo wakisema yana mlengo wa kisiasa, huku Marekani ikiishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo, lakini Rwanda imejibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe.

Aidha, kinachotarajiwa leo ni uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya upande wa mashitaka ya kuwapa kifungo cha miaka 22 washtakiwa hao, huku upande wa mawakili wao wakipinga maombi hayo na kusisitiza wateja wao kuachiwa huru mara moja.

Hata hivyo, waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini.

 

Video: Nape Nnauye alipuka, Wafanyakazi wapinga rasmi mafao mapya, Takukuru wajitosa rasmi rushwa ya ngono
Kanyasu atoa siku 30 kwa Mkandarasi wa SUMA JKT

Comments

comments