Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ limeyaalika mashirikisho yote duniani kwenye mkutano mwisho wa mwezi huu kujadili kalenda ya kimataifa, pamoja na pendekezo la Arsene Wenger la Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya miaka miwili.

Mkutano wa kwanza wa mtandaoni ni pamoja na mialiko tofauti iliyotumwa na FIFA mapema mwezi huu kwa wadau wa soka wakiwamo mashirikisho yote, Jumuiya ya Klabu za Ulaya, Jukwaa la Ligi duniani na Umoja wa Wachezaji duniani, FIFPRO.

Mada kuu ya majadiliano inapaswa kuwa pendekezo la kubadilisha kalenda ya kimataifa kwa kufanya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili, mpango ulioongozwa na kocha wa zamani wa Arsenal, Wenger, ambaye sasa ni mkuu wa maendeleo ya soka duniani wa FIFA.

“Kuna makubaliano mapana ndani ya mchezo kwamba kalenda ya mechi za kimataifa inapaswa kurekebishwa na kuboreshwa,” ilisema taarifa iliyotolewa na FIFA Jumatatu.

“Kufuatia mialiko kwa wadau, pamoja na mashirikisho yote, mwanzoni mwa mwezi Septemba, majadiliano yanaandaliwa katika wiki zijazo.

“Mnamo tarehe Septemba 15, 2021, FIFA pia ilialika vyama vyake wanachama kwenye mkutano wa kwanza mtandaoni Septemba 30, mwaka huu.”

Watu watano wafariki dunia na mmoja kujeruhiwa
Coutinho atabiriwa mazito FC Barcelona